NGUO fupi imekuwa maarufu kwa mitoko ya usiku kwa shughuli mbalimbali, na wadada wengi wamekua wakipendeza sana, lakini hata hivyo wengi wamesahau kuwa hata nguo ndefu ina umuhimu wake kiasi cha kufanya mavazi ya nguo fupi kwa usiku kama ndio utaratibu.
Ukitaka kuchagua nguo ndefu kwa ajili ya mtoko wa usiku, iwe ni sketi na blauzi,gauni, suti nakadhalika, chagua yenye nakshi ambazo zitaendana na shughuli husika.
Unaweza pia kuchagua nguo ndefu ya kubana ama yenye mpasuo mrefu kidogo, na kiatu kirefu pia.
Uchaguzi wa nguo inayotakiwa kuvaliwa, kwanza unatakiwa kuzingatia ambo mengi ikiwemo kuvaa kulingana na tukio husika, kama ni pati ya kawaida au ni kwa ajili ya sherehe fulani, uvaaji wako unatakiwa
kuzingatia rangi ya nguo na rangi ya mwili wako.
Kama wewe ni mweusi hutakiwi kuvaa nguo nyeusi kwani haitakupendeza, unashauriwa kuvaa nguo za rangi nyeupe,nyekundu, gold, bluu au njano.
Na kama wewe ni mweupe nguo ya rangi nyeusi au rangi nyingine itakupendeza kulingana na rangi ya ngozi yako.
mfano wa nguo ndefu simple ya kutokea usiku
Cha kuzingatia ni kuhakikisha kuwa nguo hiyo haikuletei tabu wakati wa kutembea kwani nguo ikiwa ndefu sana husababisha mvaaji kuishikilia na kuonekana wakati mwingine kama kituko, vaa nguo kulingana na umbo na hata urefu wako, nguo za wazi na ndefu hupendeza sana kama zitavaliwa
na mkufu au ushanga shingoni
.
Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa, unakuwa na nguo maalum ya kutokea na unatunza vizuri nguo zako kwani hilo litakusaidia kuongeza umaridadi wako na kujiamini zaidi.
Lakini pia usisahau kuwa na vipuri vitakavyosaidia vazi lako. Faida ya vazi hili, si tu kupendeza na kuonekana maridadi bali muda mwingine nguo ndefu hukufanya kuwa huru zaidi katika shughuli husika.
No comments:
Post a Comment