Una nywele dhaifu? Fanya haya kuzipa uhai..


WANAWAKE wengi hasa wale wanaopenda urembo, huangaika kutunza nywele zao
ili ziwe katika muonekano mzuri, haijalishi ni fupi ama ndefu.

Lakini kwa bahati mbaya, kuna baadhi yao wana nywele dhaifu, na ni wazi kuwa
nywele hizo huwa hazina muonekano mzuri.

Wengi wao wanadhani kuvaa wigi, ama kusuka nywele bandia kwa muda mrefu ni
suluhisho la tatizo hilo, kitu ambacho si kweli kwani nywele hizo zinatakiwa matunzo tu na
kuweka nywele bandia husababisha kuwa dhaifu zaidi.

Kama una nywele dhaifu, basi usipende kupaka rangi za nywele, kwani
kuna baadhi ni kali na hudhoofisha mara dufu, kinachotakiwa ni kufanya stiming
mara kwa mara inayoendana na nywele zako.

Unatakiwa kuwa makini katika kuchagua  mafuta pia, na kama unaona hutoweza
basi mtafute mtaalam wa nywele ili ajaribu kukusaidia kutokana na tatizo lililonalo.





Lishe nayo inahusika, jaribu kula chakula chenye virutubisho sambamba na maji mengi, hii
itakusaidia kwa kiasi kikubwa, lakini pia ni vizuri kama utachagua mafuta
yanayotokana na mimea kwa ajili ya kurutibisha nywele.

Kuweka nywele za bandia kichwani, huzifanya nywele hizo, kukosa hewa na hivyo
kunywea sana na kutofurahia urembo wako.

Kumbuka kuwa muonekano wa mwanamke kwa kiasi kikubwa ni nywele, na uwapo
na nywele asili zenye afya, bila kubandika za bandia, hukufanya kujisikia vizuri na
kuchangia furaha yako ujitazamapo kwenye kioo.

No comments:

Post a Comment