LIMAO, ni moja ya tunda lenye kazi nyingi
mwilini, lakini hapa nitalielezea kwa kazi
moja tu ya kukata harufu ya kikwapa!

Wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo
hili, na hutibu kwa njia mbalimbali, ikiwemo
kujipulizia pafyum, deodorant na marashi
mengine makali.

Kuna wenye aleji (mzio) wa matumizi ya
hivyo vitu nilivyotaja hapo juu.

Njia rahisi ya kutibu kikwapa ni hii; chukua
limao, kata vipande viwili, halafu kimoja
paka kwapa la kushoto, kwa kusugua
taratibu na kuhakikisha limeenea maji ya
limao lote, fanya hivyo katika kwapa la kulia
pia.
Kaa kwa muda wa dakika 10 halafu nenda
kaoge, hautatoa harufu hadi baada ya wiki
mbili au tatu, kisha unaweza kurudia tiba
hiyo.



Ukikosa limao, hata ndimu inahusika pia.
Kazi kwako...zipo njia nyingi za kutibu
kikwapa kwa njia ya asili, siku nyingine
nitakuletea mambo zaidi.


No comments:

Post a Comment