DIRA/DERA VAZI LA KILA MTU


NIMEKUTA mjadala kwenye moja ya mitandao kuhusu uvaaji wa magauni makubwa na mapana, maarufu kama dira/dera.

Mjadala huo, ulilenga wale wadada wanaovaa magauni hayo kwa mitindo tofauti kama vile, kuyakunja kwenye nguo ya ndani, kuvaa na mikanda nakdhalika.

Kuna baadhi walisema ni nguo za nyumbani na hazifai kutoka nazo nje, wengine waliwabeza wanaovaa nakadhalika, lakini wengi wao kwa jinsi nilivyoona michango yao, hawakulijua vazi hilo kwa undani.
Dira ni vazi la heshima, lenye kusitiri mwili wa mwanamke vizuri sana, kuliko mavazi mengine.

Kila mtu anavaa dira apendavyo, kama kwenye mtandao huo wa kijamii ulivyosema kwamba wengine wanaweka kibwewe,  wengine wanachanganya na nguo nyepesi ndani hlf inatokeza kidogo kwa chini,  wengine huvaa na mkanda au mkufu ili kulibana katikati.

Yapo ya kila dizaini na gharama tofauti tofauti kulingana na uwezo wa mvaaji, lakini huvaliwa zaidi kwenye shughuli zenye stara kama vile msibani, kwenye dua mbalimbali kwa waislam na hata vikao vya kanisani au jumuiya.

Dira linapendeza kila mtu, halikatai mwili, ni wewe mwenyewe mvaaji kuchagua rangi inayokufaa na saizi yako. Wanaodhani ni kuvaa dira ni uswahili ama ushamba, hawajui maana ya mavazi kwani hakuna vazi la mswahili wala mshamba, bali ni jinsi mvaaji atakavyopangilia mavazi yake na kuonekana nadhifu machoni pa watu.

No comments:

Post a Comment