JAPO wanja ni kipodozi maarufu sana kwa wanawake na baadhi ya wanaume
kulingana na tamaduni, lakini si wanawake wote wanatumia kipodozi hiki.
Kuna wengine hawakitumii wanja kwa sababu hawapendi, na kuna wengine wanashindwa namna ya kutumia na hivyo kujikuta wakiacha kabisa na kuendelea na kipodozi kingine.
Lakini pia kuna wanaopaka kila siku ila wanashindwa kupaka kwa namna nzuri itakayowafanya macho yao kukaa kwa uhalisia unaotakiwa. Basi ni vyema kama unapenda kutumia kipodozi hiki cha jicho ukajifunza
namna nzuri ya kukitumia.
Macho madogo
Paka wanja kwa kukoleza sehemu ya juu ya jicho (ngozi iliyozunguka kope), halafu zungusha hadi chini ya jicho taratibu. Paka mwanzo wa jicho hadi mwisho kwa umakini mkubwa bila ya kuchafua sehemu
isiyohitajika.
Koleza kwa kurudia rudia, ama unaweza ukaanza na rangi nyingine halafu ukapitiasha wanja mweusi juu itasaidia kukoza zaidi, na hii itakufanya jicho lako kuonekana kubwa kidogo.
Macho makubwa
Unaweza kupaka kama jinsi macho madogo yanavyopakwa na hii itakufanya
jicho lako kuwa kubwa zaidi ama kama hautapenda waweza kupaka kama
ambavyo nitaelekeza hapa chini.
Paka wanja kwa kuzungusha juu na chini lakini si kwa kukoleza sana, na
ama unaweza kutumia rangi za giza kabla ya kupaka wanja mweusi na
halafu baada ya kumaliza paka poda kupunguza wanja uliozidi.
Baada ya hapo waweza paka shadow yoyote ya macho uipendayo kulingana
na mahitaji yako.
No comments:
Post a Comment