MANUKATO YA UDI


KWA kawaida mwili wa mwanamke, baada ya kupambwa vizuri hunakshiwa na harufu nzuri ya marashi. Marashi hayo huweza kuwa pafyum za aina mbalimbali na ama udi.

Kuna watu wengi pengine wangependa kutumia udi lakini wanashindwa kufanya hivyo kutokana na kutojua namna ya kutumia ama kutokana na ugumu wa matumizi yenyewe.

Siku hizi mambo yamerahisishwa, na hapa nakuletea dondoo chache za namna ya kutumia manukato hayo kwa njia mbalimbali ambazo utazimudu.

Kwanza kabisa, kuna udi ambao umewekwa kwa mtindo wa marashi (pafyum ya udi) kutoka kiwandani, basi hapo waweza chagua yenye harufu kali ama inayonukia kwa mbali.




Kwa marashi ya udi yenye harufu kali ni vyema kama utaweka katika nguo siku mbili kabla ya kuvaa halafu wakati wa kuvaa  ukatumia yale yenye harufu ndogo mwilini.

Kwa udi wa kufukiza, kuna chetezo cha umeme, na udongo kinachotumia makaa.



Kwa chetezo cha udongo, chukua stuli yenye nafasi ya uwazi chini, kisha ilaze chini juu halafu tumbukiza chetezo chenye moto na mwagia udi humo, halafu weka nguo yako kwa juu (husaidia isiungue ama kuwa na rangi ya njano inayotokana na moshi.) Geuza geuza nguo na ukiridhika kama imekolea marashi itoe na zima moto.

Kwa chetezo cha umeme, tafuta stuli, ama kifaa kirefu kisha tundika nguo, na weka udi katika chetezo kisha chomeka kwenye umeme. Geuzageuza nguo na ukiridhika zima chetezo.

Waweza pia kufukiza katika kabati la nguo na hii itakupa urahisi hata siku ukiwa na haraka kuendelea kunukia bila kujifukiza. 

No comments:

Post a Comment