Nilibahatika kuwepo, pamoja na mambo mengine nilikuwa naangalia mitindo ya nywele, nguo hadi viatu..bila kusahahu accesories..na hawa ni baadhi tu ya walionivutia.
Irine Uwoya, kwa kweli alipendeza saaaana, tena naweza kusema kuliko wengi kama sio wote waliofika. Alivaa kiafrika, na kitenge kilimkaa mnoo..mtindo wa nywele simpo, na hakujiza makeup usoni...dooh alitoka mwake mwake
Penny...mama Diamond alitoka kiasi chake..alichanganya African Print na mikogo ya nje..nywele simple ila makeup kidoogo ilizidi, ila sio mbaya
NI HAYO TU KWA LEO
No comments:
Post a Comment