KIKUKU PIA NI UREMBO


UVAAJI wa vikuku (cheni au shanga za miguuni) ni pambo maarufu kwa
wanawake lakini limekuwa likitafsiriwa katika maana mbaya.

Vikuku si kitu kigeni kabisa, kwani ni urembo uliokuwa unavaliwa na makabila
mengi hapo nyuma, lakini kwa miaka ya hivi karibuni, umeboreshwa zaidi.



Kwa kawaida mwanamke ni mtu anayepemba kujiremba na kujipamba kwa namna yoyote
atakayoona inafaa, na hata kikuku ni sehemu ya urembo huo.

Kikubwa ni dhamira ya mvaaji na uhuru alionao katika kuvaa urembo husika, iwe
hereni, bangili, pete nakadhalika.

Sasa, kazi kwako, jimwage upendavyo na kikuku, kwani vipo vya bei tofauti na
thamani tofauti na vinavyotokana na madini tofauti.

Na katika hili sio masihara hata kidogo, kikuku kinapendezesha mguu hasaaa, na
kama unajua kuutunza huo mguu, raha yake utaiona shosti.

No comments:

Post a Comment