Unadhifu ni pamoja na meno


UMARIDADI na usafi haumaanishi kuwa na muonekano mzuri wa nje pekee,
bali kila kiungo ndani ya mwili kinahusika.

Wengi, wamekuwa wakidhani kuweka uso safi ni kitu kinachotosha katika
muonekano kwanza, la hasha bali ukweli ni kuweka vyote vinavyoonekana
usoni safi kisha maeneo mengine kufuata.

Muda mwingine mtu anaweza kupendeza sana na uso akauremba vizuri
lakini akicheka meno yake ya njano, yana mabaki ya chakula ama muda
mwingine kutoa harufu mbaya kabisa, mpaka hapo urembo wake unakuwa
hauna maana tena.

Kusafisha meno ni kitu kidogo lakini chenye umuhimu mkubwa. Kutokana
na ukweli kwamba kuna baadhi ya maeneo hayafiki mswaki sawasawa, ama
tu umakini kutoka moyoni ni vizuri kusafisha kinywa kwa uzi maalum wa
kutolea mabaki ya chakula.

Namna ya kufanya

 Toa mabaki ya chakula kwenye meno kwa kutumia uzi maalum angalau
mara moja kwa siku baada ya kusugua meno asubuhi ama usiku kwa
kuingiza katikati ya jino na jino ukiwa na maji safi pia kwa ajili ya
kusukutua.

Tumia uzi wa aina yoyote msafi na mweupe  na wenye nta ndio utakuwa
rahisi zaidi kutumia. Kata  nusu mita kisha ujifunge kwenye kidole kwa
mkono moja. Funga sehemu ya mwisho kwa kidole cha mkono wako wa pili.

Shikilia uzi huo kwa nguvu kwa vidole vyako halafu pitisha katikati
ya meno yako kwa upole kwa kukwaruza polepole juu na chini. Uzi
ukikuchafuka, badilisha mwingine msafi.

 Rudia mara ya mwisho katika kila sehemu ya katikati ya meno yako hadi
sehemu ya mwisho ya meno na ukiridhika a usafi wake, waweka pitisha
mswaki juu na kunawa kwa usafi

No comments:

Post a Comment