ASALI HUKABILIANA NA UZEE
Asali ina matumizi mengi sana, japo huliwa katika chakula, na kutumika kama tiba kwa baadhi ya
magonjwa, lakini pia ina mchango mkubwa sana katika urembo.
Pamoja na kusaidia katika ngozi kwa suala la urembo kwa ujumla, lakini pia asali ina vimeng'enya vinavyosaidia kukabiliana na uzee.
Ili ifanye kazi kwa matokeo mazuri, anza kutumia kama moisturize ajili
ya uso na ngozi ya mwili kwa ujumla, kwani inasaidia ngozi ya majimaji na kukufanya kuwa laini muda wote. Inadaiwa kuwa ina uwezo wa kukusanya maji kutoka ndani ya misuli hadi katika sehemu za juu za ngozi na hivyo kusaidia kuondoa mikunjomikunjo.
Jinsi ya kufanya
Changanya vijiko viwili vya mezani vya asali na vijiko viwili vya
mezani vya maziwa, baada ya hapo pasha moto mchanganyiko huo halafu
paka usoni, na acha dakika kumi au robo saa.Kisha osha na maji ya uvuguvugu na si ya moto kabisa.
Tumia pia bidhaa zinazotengenezwa kwa asali kulingana na ngozi yako kama Bee Ceuticals Organics’ Honey Thyme Hand na body lotion ambayo imetengenezwa kutokana na asali iliyochujwa.
Matumizi ya aina yoyote ya asali yanasaidia kuondoa mikunjo ya uzee.Kwenye matumizi mengine ya kawaida ni pamoja na kuweka kwenye mkate,kutumia kama kiungo kwenye chai nakadhalika.
Asali ni njia nzuri ya asili ya kuboresha ngozi na isiyo na gharama kubwa wala madhara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment