Kuondoa chunusi kwa kutumia manjano

MIMI ni fan wa page ya Shear Illusions, facebook..katika pita pita za kuangalia posts kwenye ukurasa huo nikakutana na hii...nikaona ni vyema nikashare na wadau wa blog hii ambao hawajabahatika kukutana na utaalam huu.

Mahitaji  ya kuondoa chunusi kwa manjano


- Vijiko viwili (2 tbs) vya unga wa binzari ya Manjano (Turmeric powder)
- Kijiko kimoja (1 tbs) cha unga wa Riwa - wengine huita Liwa (Sandalwood)
- Vijiko vinne (4 tbs) Maji masafi
- Nusu kijiko (1/2 tbs) cha mafuta ya Haradali (Mustard Oil)
- Kijiko kimoja (1 tbs) cha maji ya ndimu/limao (Lemon juice)















Jinsi ya kufanya

Safisha uso wako kwa sabuni uwe msafi. Changanya vyote kisha upake usoni (kasoro eneo lililozunguka jicho). Kaa nayo usoni mpaka ikauke au kwa muda wa dakika 15. Kisha nawa uso wako kwa
maji ya kawaida – usitumie sabuni. Fanya hivi mara 3 kwa wiki na utaona mafanikio ya chunusi kuisha.



Kama una chunusi nyingi sana chukua glasi moja ya maziwa ‘fresh’; weka kijiko kimoja (tea spoon) cha
unga wa binzari ya Manjano, koroga na unywe - kunywa mara 3 kwa wiki (sio kila siku) - Itasaidia kuboost ‘immunity’ yako na pia kuisaidia system yako mwilini katika kutibu chunusi.

Haya, hangaika nayo mwenyewe..shukran nyingi kwa shear illusions


2 comments:

  1. Hello asante sana kwa kushare nasi taarifa hii kususiana na matumizi ya manjano....
    Ila naomba kuuliza je kama huna mafuta ya haradali inakuwaje kuhusu hii recipe ya uso?

    ReplyDelete
  2. Tatizo hivyo vitu vingine ni ngumu kuvipata mf mafuta ya haradali,liwa ni ngumu ndugu labda mtu kujiongeza na mchanganyiko mwengine..

    ReplyDelete