Limao na sukari hutibu weusi chini ya macho na kwenye viungio vya mwili

Zipo njia nyingi za kuondoa weusi katika maungio na sehemu za ndani, mfano kwapa, chini ya macho nakadhalika.Njia hizo huwa ni za asili ama kwa kutumia vifaa vilivyotengenezwa viwandani.

Sehemu hizi zinapokuwa nyeusi, huwanyima raha wanawake hasa katika suala zima la mavazi, kwa mfano mwenye weusi makwapani, hushindwa kuvaa nguo ya kata mikono, au mwenye weusi katika magoti hushindwa kuvaa kimini kwa kuhofia weusi huo kumuondolea urembo.

Leo,  nitakwambia  namna ya kuondoa weusi katika kwapa kwa kutumia limao na sukari.



Limao, licha ya kuzuia jasho na harufu ya kwamba, lakini pia husaidia kuondoa weusi kwa haraka, na unachotakiwa kufanya ni kuchukua kipande cha limao, halafu weka sukari kidogo, sugua.

Hakikisha umesafisha kwapa ndipo umeanza tiba hii, sugua kabla ya kuoga na baada ya kuoga.Unaweza pia kutumia limao kwa kuondoa weusi unaotokana na chunusi usoni au magotini. Ni njia rahisi isiyogharimu fedha wala muda, lakini pia haina madhara kwa mtumiaji.
 
Ukitumia njia hii huna haja ya kutumia deodorant, kwani ni zaidi ya bidhaa hiyo, na  ni vizuri ukiwa unarudia mara kwa mara.

Zipo njia nyingi za asili, kazi kwako kutembelea blog hii ili uzidi kufaidi..na wewe kama unacho cha kwako kwa ajili ya kushare na wenzio, nitumie rabia.bakari@gmail.com

No comments:

Post a Comment