Ngozi ngumu? Jaribu tiba hii


UREMBO wa mwili haumaanishi mavazi na vipodozi pekee, bali huanza
kubebwa na ngozi ya mwili kwa ujumla pamoja na uangalizi wa hali ya
juu wa viungo.


Kutokana na ukweli huo basi, ndio maana ukiwa na ngozi ngumu
iliyopitiliza ni wazi kuwa urembo wako utakuwa na kasoro mahali fulani na
hata kuna baadhi ya mavazi hayatokupendeza. Mfano nguo inayoacha wazi sehemu kubwa ya
mwili.

Namna nzuri ya kufanya kwa wale wenye ngozi ngumu, hususan endapo
unataka kuvaa nguo itakayokuacha wazi mwili mzima ni vyema ukatumia
'scrub' ya asali na nyanya.

Hata kama unatumia scrub ya aina nyingine lakini hii ya asili ina
manufaa hasa pale ambapo unakuwa na dharura kwani huwa na matokeo ya
muda mfupi.

Jinsi ya kufanya



Chukua nyanya iliyoiva, imenye kisha iponde iponde na baada ya hapo
osha mwili wako vizuri na upake katika sehemu utakayoacha wazi, mfano
kama miguu na mgongo,  paka nyanya uliyoponda kwa kusugua taratibu na
ikishakolea  eneo lote chukua asali upake kama ulivyo fanya wakati wa
kupaka nyanya.


Acha ikauke kwa robo kisha kaoge  na uendelee na mafuta unayotumia.
Kwa matokeo mazuri tumia mara mbili kwa wiki.
Alamsiki..

No comments:

Post a Comment