Si lazima kumechisha


INGAWA kumechisha kupo kwenye chati katika suala zima la urembo, mitindo na mavazi, lakini hilo halizuii ladha ya rangi mchanganyiko.

Kumechisha, kumekuwa  ni kama kanuni, ili kujiweka maridadi zaidi, ila kwenye mitindo, unaweza kuwaza zaidi katika hilo.

Mtindo wa mavazi ya rangi rangi,zamani ilikuwa ikionekana kama kituko, lakini ukweli ni kwamba rangi hizi zikipangiliwa vizuri mwilini, huvutia.



Kwa sababu, licha ya kumechisha kwa rangi zinazofanana, lakini pia kiasili kuna rangi ambazo zikichanganywa pamoja kwa mpangilio mzuri, huwiana na kupendeza sana.

Kwa hiyo, mitindo, pia wabunifu wa mavazi wamejaribu kuzitumia rangi hizo vizuri na kumfanya mvaaji
kuonekana kama ua machoni mwa watu.

Unaweza kuchanganya rangi hizi kuanzia katika viatu, mavazi, vipuri, mkoba na hata ya rangi ya nywele, kwa kadri utakavyoona inafaa, na isikupe shida sana.

Muhimu ni kuzingatia kwamba, rangi utakazochanganya kwanza zinaendana, katika mpangilio wa rangi, na pia zinaendana na rangi ya mwili wako.



Pia wakati ukiamua kuvaa kwa kuchanganya rangi, angalia tukio husika, na aina ya mavazi yanayotakiwa, kwani itakusaidia kukuweka huru na pia kwenda na wakati kwa muda husika.

Si vibaya basi, nawe siku moja moja ukajinogesha kwa kuchanganya rangi katika mavazi, hasa katika sherehe ambazo zinaruhusu kujiachia kwa namna mtu apendavyo.

No comments:

Post a Comment