Matumizi ya cream ya mchana na usiku


WENGI, tumezoea kutumia kipodozi cha aina moja kwa matumizi yote, yaani  kazini mchana, kwenye mitoko ya kawaida, harusi nakadhalika.Ingawa wengi wanabadilisha 'makeup', lakini si kwa kiasi kikubwa matumizi ya 'cream'.

Kuna madhara makubwa ya kupaka kipodozi cha usiku wakati wa mchana na cha mchana wakati wa usiku, hivyo kama unaipenda ngozi yako ni muhimu kuwa makini katika hili.

Aina ya cream za usiku                                
                                            


   
Kwanza zinasaidia  kuirudisha ngozi katika hali yake ya kawaida, kuifanya kuwa imara, na kutibu sehemu ambazo zimeharibika kwa sababu ina vitu ambavyo vinaipa ngozi uhai  kama Retinol na vitamin C.

Ukienda katika maduka ya vipodozi utapatiwa aina nyingi ya cream za usiku kulinga na ngozi yako.

Cream za mchana



Hizi moja kwa moja zimetengenezwa kukabiliana na madhara ya jua, vumbi pamoja na hali ya hewa yote ya mchana, na ina 'Hydrate' ambapo inafanya ngozi yako iwe ya kupendeza na kung'aa wakati wa mchana.

Cream za mchana zinasaidia ngozi iwe na afya, na kukabiliana na hali yoyote ya ngozi ikiwemo  'stress'  na zinasaidia kuongeza kinga ya ngozi. Zinasaidia vitundu vya hewa kuwa wazi na kupumua, pamoja na kusaidia kuondoa mikunjamano katika maeneo ambayo ni rahisi kuathirika na vipodozi kama uso na ngozi izungukayo macho.

Hivyo basi kwa kuwa cream ya mchana ina kazi tofauti na ya usiku, ni wazi ukichanganya
matumizi kuna hatari ya ngozi yako kuharibika mapema. Cream ninazozungumzia hapa ni zile ambazo hazina madhara kwa ngozi wala kemikali zenye sumu.

No comments:

Post a Comment