Yafahamu madhara ya kufanya pedicure mara kwa mara

Wanawake wengi, hata baadhi ya wanaume, wamekuwa na kawaida ya kuosha miguu kwa vifaa maalum hasa katika saluni (PEDICURE).

Wengine, wamekuwa wakifanya hivyo, karibu kila wiki ama kila baada ya siku kadhaa kutokana na kuijali miili yao na muoenekano pia.

Ukweli umejificha katika hili, na wengi wetu nadhani hatuujui.

               
Leo niliingia saluni moja ya kike iitwayo CANDRA  kwa lengo la kuosha miguu, wakati wa maongezi ya hapa na pale, ndipo waliponishauri kuosha miguu mara kwa mara kuna madhara.


Mtaalamu wa kuosha miguu na kutengeneza kucha katika saluni hiyo, Fairuna Rashidi, akanipa ushauri ambao nimeona ni vyema kushare na wenzangu.

Anasema kuwa, kuosha miguu, ambako kunahusisha kuondoa ngozi ya miguu iliyokufa kwenye nyayo, mara kwa mara, kunadhoofisha ngozi hiyo na hatimaye kukuletea maradhi.

Maradhi hayo ni pamoja na miguu kuwaka moto, kuuma na hata kushindwa kutembea kwa mwendo mrefu, kwani kadri unavyoondoa ngozi iliyokufa, unadhoofisha ngozi asili ambayo Mwenyezimungu aliiumba kusudi ikinge madhara mbalimbali kwenye miguu.

Hivyo basi, Fairuna anashauri angalau osha miguu yako mara moja kwa wiki mbili, kwa wale wenye miguu yenye matatizo ya ukavu, kutembea kwenye vumbi na misukosuko mingi, lakini kwa wale wenye ngozi ya kawaida basi ni vyema angalau mara moja kwa mwezi.

Anasema madhara hayo hutayaona haraka, bali itakuja kukutokea miaka kadhaa mbeleni.




Haya pamoja na ushauri huo ambao ulinifaa sana, lakini pia saluni ya CANDRA ni watengenezaji wazuri wa nywele, kusukia weaving aina zote kwa bei nafuu, pia wanauza nguo, viatu, vipodozi na huduma nyingi kwa ajili ya mtoto wakike.

Kwa matengenezo ya kucha muone Fairuna 0658 80 81 11
Kwa mahitaji ya kutengeneza nywele mtwangie Whitness 0716 242614

Wapo Kinondoni Road, wanapakana na Bank ya Barclays ama wanatizamana na kanisa la Pentecoste.Wanafungua saa tatu asubuhi na kufunga saa mbili usiku.
Waone kwa huduma bora

No comments:

Post a Comment