UMARIDADI MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

 
Kama inavyojulika, mwezi huu ni mtukufu, na mavazi yake yanatakiwa kuwa matukufu
vilevile. Kwa wale wanawake wanaopenda kwenda na wakati ni vyema wakatafuta
mavazi ya fasheni lakini yanayoendana na mwezi huu.
 
Mfano, unaweza kuvaa dira lililodariziwa vizuri na mtandio mwepesi ambayo
utakufanya uonekane mrembo, pia kuna mabaibui yenye nakshi nzuri vile vile
yatakayokufanya upendeze pia huku ukiwa umejisitiri mwili vizuri.
   

Pia unaweza kuvaa gauni refu au sketi na blauzi ndefu, kisha ukachukua mtandio
mdogo na ukaenda sambamba na wenzio katika mfungo huu.


 Japo mavazi haya ni kwa waislam, lakini yamekuwa yakimpendeza kila mmoja, hivyo
si mbaya kwa wale wapenda mitindo pia wakabadilika mwezi huu na kwenda
sambamba na waislam.

No comments:

Post a Comment