VAZI LA ABAYA

KATIKA mwezi huu mtukufu, mavazi marefu na yenye heshima ndio yamekuwa
yakipewa nafasi kwa kiasi kikubwa, na hasa kwa waumini wa dini ya
kiislam.

Pamoja na hayo, marafiki wengi, na hasa wapenda mitindo nao wamekuwa
wakienda sambamba na marafiki wa kiislam na hata kuifanya miji
kupambwa na mavazi marefu yenye nakshi mbalimbali.

Mojawapo ya mavazi yaliyoshika kasi mwezi huu ni vazi  la Abaya,
ambalo limekaa kama baibui lakini lina nakshi za pekee na pia linaweza
kuwa wazi kwa mbele ama kufunika kote.



Abaya linaweza kuwa kama mtandio, ambao ukijitanda kichwani na
kufunika mwili mzima, na pia linaweza kuwa la kitambaa chepesi, ama
kizitoi wastan bali haipendezi ikishonwa kwa kitambaa kizito zaidi.

Abaya ni vazi lenye thamani sana, kwani bei yake ni tofauti na baibui
la kawaida, lakini pia uzuri wa vazi hili, ni la heshima na
lisilopitwa na wakati.



Unaweza kuona katika picha namna abaya linavyoweza kumnakshi mwanamke
na kumfanya kuwa kama pambo.

Basi si vibaya, nawe ukajitahidi angalau upate moja, ili uweze
kujinakshi katika mwezi huu na hata baada ya mwezi kwisha, kwani kama
nilivyosema, abaya ni vazi lisilopitwa na wakati.

No comments:

Post a Comment