Lipstick na upakaji wake


Kila kiungo katika mwili wa mwanadamu kinahitaji kuangali, kuwekwa vizuri na kupendezeshwa hasa kwa mwanamke.
Midomo, ambacho ni kiungo muhimu sana kwa mwanadamu kinahitaji kutunzwa na kurembwa.
Ngozi ya midomo ni laini sana na kipodozi kikubwa kwa ajili yake ni lipsticik, lipbam, lipshine na vitu kama hivyo.



Kwa wanaopaka lipstick, angalia namna rahisi ya kupaka kipodozi hicho na utoke mwake mwake.
Anza kwa kutafuta brush ya kupakia lipstick, kisha chovya kwenye lipistick kisha fumba midomo na inua mbele kidogo, na anza kupaka taratibu.
Ukimaliza chukua kitambaa na ufute sehemu iliyozidi hlf malizia na kipodozi chochote juu kisha kama unapenda ing'ae sana waweza ongeza na lipgloss ili kung'arisha.


No comments:

Post a Comment